Tarehe 07.12.2023 mwaka wa Bwana katika nyumba ya malezi parokia ya Chala
Katika picha ni Masista 16 wa nadhiri za kwanza wa shirika la Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika-Jimbo la Sumbawanga 07.12,2023
Adhimisho la Misa Takatifu limefanyika katika Kanisa la Nyumba ya malezi ya Shirika hilo, iliyopo Parokia ya Mtakatifu Fransisco wa Sales – Chala Jimbo Katoliki Sumbawanga. Ikiwa ni utangulizi wa sherehe za Shirika hilo, ambazo hufanyika tarehe 08.12. au maarufu Nane Disemba Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi(Emakulata).
Adhimisho la Misa Takatifu limeongozwa na Askofu Emeritus Damian Kyaruzi wa Jimbo la Sumbawanga, Na aliyepokea Nadhiri 16 za kwanza kwa Masista 16 ni Mama Mkuu wa Shirika hilo Mheshimiwa SR. Editruda Mbegu Mbele ya Mhashamu Baba Askofu Damian Kyaruzi, ambaye amemwakilisha askofu wa Jimbo Mha, Beatus Urassa ALCP/OSS.
Katika sherehe hizo za nadhiri za kwwanza wameudhuria , watu mbalimbali wakiwemo mapadri, watawa waamini wakinogeshwa na furaha ya walelewa amabo wameshuhudia safari ya dada zao ikifika mwisho katika hatua msingi ya nadhiri za awali tunawaombea udumifu mwema
Katika picha hapo chini ni mnadhiri mpya wa nadhiri za kwanza Sista Maria Nzunda kutoka parokia ya Tunduma jimbo katoliki Sumbawanga
Sherehe ya Bikira Maria Kupashwa Habari kuwa atakuwa ni Mama wa Mungu kwa mwaka 2024 inaadhimishwa Jumatatu tarehe 8 Aprili 2024, baada ya tarehe 25 Machi 2024 kuangukia kwenye Juma Kuu. Tarehe 8 Aprili 2024 Mama Kanisa sehemu mbalimbali za dunia anaadhimisha Siku ya Kutetea Uhai na Utakatifu wa Maisha tangu pale mtoto anapotungwa mimba…
Baba Mtakatifu Francisko anasema, huruma ndiyo msingi thabiti wa uhai wa Kanisa. Kazi zake zote za kichungaji zinapaswa kufungamanishwa katika upole linalouonesha kwa waamini; hakuna chochote katika mahubiri na ushuhuda wake kwa ulimwengu kinachoweza kukosa huruma. Umahiri wa Kanisa unaonekana kwa namna linavyoonesha huruma na upendo. Huruma ya Mungu inafungua malango ya moyo ili kuonesha…
Matukio Katika Picha ni wakati wa adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu ya kutolewa kwa Daraja ya Ushemasi iliyofanyika katika Parokia ya Epiphania Kanisa Kuu Jimbo Katoliki Sumbawanga, misa iliyoadhimishwa na Mhashamu Beatus Christian Urassa Askofu wa Jimbo Katoliki Sumbawanga. waaliowekwa wakfu katika Daraja Takatifu ya Ushemasi Jimboni Sumbawanga hii leo ni pamoja na; ▪️Shemasi…
Likizo ni nafasi muafaka ya kujenga na kudumisha mahusiano na mafungamano ya dhati na Mwenyezi Mungu, kwa kusoma na kutafakari Maandiko Matakatifu, lakini zaidi kwa kuongozwa na Amri Kumi za Mungu kama dira na mwongozo wa maisha. Ni nafasi ya kutafakari kuhusu Fumbo la maisha ya binadamu, ili kubainisha ikiwa kama maisha yana alama na…
Na. Pd Joseph Luwela-Vatican-Roma Utakatifu ni mchakato unaowawezesha waamini kuishi upendo katika utimilifu wake kadiri ya nguvu na mwanga wa Roho Mtakatifu. Maisha ya kila mwamini yawe ni kielelezo cha utume kutoka kwa Kristo Yesu anayetaka kuwaletea waja wake mabadiliko katika maisha, licha ya udhaifu na mapungufu yao ya kibinadamu, daima wakijitahidi kuambata upendo wa…
Kipindi cha Kwaresima ni fursa ya kuamsha na kupyaisha ari na mwamko wa kimisionari, tayari kujisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu hadi miisho ya dunia. Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini kuwakumbuka na kuwaombea wainjilishaji wote, ili waweze kuwa ni vyombo na mashuhuda wa kile wanacho amini, kufundisha…