Mapokezi ya Mwadhama Polycarp Kardinal Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dsm, alipowasili Jimbo Katoliki Shinyanga katika ziara za kichungaji, mnamo tarehe 6.12.2023.
Katika picha ni baadhi ya waamini wa jimbo katoliki la Shinyanga wakiwa na nyuso za furaha wakimkaribisha Kardinali Pengo katika mipaka ya jimbo hilo
Mha Askofu Sangu aongoza mapokezi na kumkaribisha Mwadhama kadinali Pengo jimboni humo kwa ziara ya kichungaji kuanzia tar 06.12.2023
Mama Kanisa katika masomo ya dominika hii anatukumbusha kuwa kwa Sakramenti ya Ubatizo na kipaimara sisi sote tumeitwa kuihuburi Injili kwa kuishi ukristo wetu vyema sio kwa sheria za maumbile bali kwa kuwa viumbe vipya ndani ya Kristo na kuona fahari juu ya Msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambao kwao tumekombolewa. Hii ni changamoto…
Kipindi cha Kwaresima ni fursa ya kuamsha na kupyaisha ari na mwamko wa kimisionari, tayari kujisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu hadi miisho ya dunia. Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini kuwakumbuka na kuwaombea wainjilishaji wote, ili waweze kuwa ni vyombo na mashuhuda wa kile wanacho amini, kufundisha…
Baba Mtakatifu Francisko anasema, huruma ndiyo msingi thabiti wa uhai wa Kanisa. Kazi zake zote za kichungaji zinapaswa kufungamanishwa katika upole linalouonesha kwa waamini; hakuna chochote katika mahubiri na ushuhuda wake kwa ulimwengu kinachoweza kukosa huruma. Umahiri wa Kanisa unaonekana kwa namna linavyoonesha huruma na upendo. Huruma ya Mungu inafungua malango ya moyo ili kuonesha…
Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 5 Aprili 2024 amekutana na kuzungumza na Jumuiya ya Ndugu Wadogo wa La Verna na wale wanaotoka Kanda ya Toscana, kama sehemu ya kumbukizi ya miaka mia nane tangu Mtakatifu Francisko wa Assisi alipobahatika kupewa Madonda Mtakatifu mwilini mwake. Hii ilikuwa ni tarehe 15 Septemba 1224, yaani miaka miwili kabla…
Sherehe ya Bikira Maria Kupashwa Habari kuwa atakuwa ni Mama wa Mungu kwa mwaka 2024 inaadhimishwa Jumatatu tarehe 8 Aprili 2024, baada ya tarehe 25 Machi 2024 kuangukia kwenye Juma Kuu. Tarehe 8 Aprili 2024 Mama Kanisa sehemu mbalimbali za dunia anaadhimisha Siku ya Kutetea Uhai na Utakatifu wa Maisha tangu pale mtoto anapotungwa mimba…
katika picha ni Masista wa , Jubilei ya miaka 25 ya Utawa kwa Masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika (MMMMA), Jimbo Katoliki Sumbawanga. Adhimisho la Misa Takatifu limefanyika Parokia ya Epiphania Kanisa Kuu Jimboni humo. Jubilei ya miaka 50 Aliyeadhimisha Misa Takatifu ni Mhashamu, Damian Kyaruzi, Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki Sumbawan, na aliyepokea…